Soka na maajabu yake, mchezaji wa Klabu ya Mbao FC, Emmanuel Elias Mseja, amepigwa faini ya Sh. 100,000 na kufungiwa mechi tatu baada ya kujisaidia-kukojoa uwanjani wakati wa mchezo kati ya timu yake dhidi ya AFC iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
Msemaji wa TFF, Baraka Kizuguto, amesema mbali na adhabu hiyo, nao pia viongozi wa Mbao Abdallah Chuma (daktari) na meneja wao Yasin Abdul wamefungiwa miezi sita na kutakiwa kulipa kitita cha 100,000 kila mmoha kwa kumtukana na kumtishia maisha kamishna wa mchezo huo.
Nayo klabu ya AFC imepigwa faini ya sh. 300,000 kutokana na washabiki wake kuifanyia vurugu timu ya Bulyanhulu FC kwenye mechi yao iliyofanyika Februari 7 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Timu ya Magereza Iringa imepigwa faini ya jumla ya sh. 200,000 kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting), na uwanjani kwenye mchezo wao na Njombe Mji uliochezwa Februari 21 mwaka huu. Naye mchezaji wa timu Amasha Mlowasa amefungiwa mechi tatu na faini ya sh. 100,000 kwa kumtukana mchezaji mwenzake kwenye mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment