Timu za Ujenzi Rukwa na Volcano FC ya Morogoro zimeshushwa madaraja mawili hadi ligi za wilaya baada ya kushindwa kufika uwanjani kwenye mechi zao za Ligi Daraja la Pili (SDL).
Uamuzi huo umefanya na Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana jijini Dar es Salaam kupitia ripoti za matukio mbalimbali ya ligi hiyo.
Ujenzi Rukwa ilishindwa kwenda Kigoma kuikabili Mvuvumwa FC ya huko wakati Volcano FC haikutokea kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo ilitakiwa kucheza na Wenda FC.
Uamuzi wa Kamati ya Mashindano umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 27 ya SDL ambapo mbali ya kushushwa madaraja mawili, lakini pia timu hizo zimepigwa faini ya sh. milioni moja kila moja. Vilevile matokeo yote ya mechi zao kwenye Ligi hiyo yamefutwa.
Nayo Singida United imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Ujenzi Rukwa kubainika kumchezesha mchezaji asiyestahili (non qualified) kwenye mechi iliofanyika Februari 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1
No comments:
Post a Comment