Tuesday, March 3, 2015

TIKETI ZA KIELEKTRONIKI ZAPIGWA STOP TAIFA

Marufuku kukanyaga taifa...mfano wa tiketi za kielektroniki zilizopigwa stop kwenye Uwanja wa Taifa kuanzia leo.
Serikali imesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia leo (Machi 3, 2015) hadi kasoro zilizopo katika matumizi ya tiketi hizo zitakapoondolewa.
Uamuzi huo umetangazwa leo (Machi 3, 2015) jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Juma Nkamia mbele ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB.
sasa ni mwendo wa mfumo wa ki-analogia, baada ya kushindwa kuendena na kasi ya digitali
Kabla ya maamuzi hayo, klabu nyingi zimekuwa zikilia na mfumo huo ambao ulianza kutumika msimu uliopita lakini ukasimamishwa katikati kutokana na kubaini kuwa ulikuwa na changamoto nyingi ikiwemo suala la kuweka foleni kutokana na mashine kuchelewa kama sio kushindwa kusoma kabisa tiketi.
Benki ya CRDB ndiyo ilishinda tenda ya kutengeneza tiketi hizo.
Changamoto kubwa ambayo imekuwa ikilizwa zaidi na takribani kila timu ni kupungua kwa mapato na hii ilihofiwa kutokana na mashabiki kukacha kwenye viwanjani kutokana na mchakato wa kupata tiketi yenyewe kuwa mrefu na usumbufu mkubwa.
Kwa Mantiki hiyo, mchezo wa Jumapili kati ya Simba na Yanga mfumo utakaotumiwa ni tiketi za zamani- zinazopatikana kwenye vituo maalum  pamoja na magari maalum pale uwanjani.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...