Thursday, February 19, 2015

YANGA YAWEKA REKOD MPYA SOKOINE BAADA YA MIAKA ZAIDI YA 5, AZAM YABANWA NA 'MASAU BWIRE'


Baada ya kukabana kileleleni kwa muda mrefu, hatimaye mabingwa wa kihistoria kwenye ligi ya Tanzania, Yanga leo wamekaa kileleni rasmi baada ya ushindi mnono wa mabao 3-0 kwa kuichapa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine.

Mabao ya mawinga, Andrey Coutinho na Simon Msuva aliyefunga mawili, yameifanya Yanga kufikisha pointi 28, mbili zaidi ya Azam ambao wamebanwa mbavu ya Maafande wa Ruvu Shooting ya msemaji mwenye mbwembwe, Masau Bwire, kwenye Uwanja Mlandizi, Pwani.
NUKUU MUHIMU

"Ushindi wa Yanga wa leo ni kwanza, yapata miaka zaidi ya miaka sita kwenye Uwanja wa Sokoine, ambapo huku zikionesha Yanga haijashinda pointi yoyote zaidi ya kutoa sare 2008/9, 2012/13, 2013/14 kabla ya kufanya kweli leo.
. Msimu uliopita, Yanga ikiwa chini ya Mholanzi, Ernie Brandts, ilipata pointi mbili tu kati ya sita, baada ya kulazimishwa sare katika mechi zote; dhidi ya Prisons na Mbeya City.
. Ushidi wao, umemfanya kocha Pluijm kuvunja mwiko wa pili klabuni hapo, kufuatia ya hivi karibuni kupata ushindi wa kwanza, baada ya miaka sita kwenye Uwanja wa Jamhuri ikiwa mara ya mwisho Yanga iliifunga Mtibwa kwa mabao 2-1 mwaka 2009."


Mabingwa Azam wamekuwa kileleni mwa muda mrefu wakikabana koo na Yanga kwa kulingana pointi, lakini wao wakiwazidi mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo ushindi wa wapinzani wao umewashusha rasmi.

Msuva alianza kuifungia Yanga kunako dakika ya nne akimalizia kwa kichwa mpira wa kona iliyochongwa na Mbrazili, Coutinho, kabla ya Coutinho kuandika bao la pili dakika ya 12 kwa kuunganisha mpira wa Amisi Tambwe uliogonga mwamba na kurudi uwanjani.

Msuva alihitimisha kalamu ya mabao kwenye mchezo huo, kwa kuunganisha tena kwa kichwa mpira wa kona iliyochongwa na Coutinho katika dakika ya 62

Katika Uwanja wa Mlandizi, licha ya kuwa na nahodha wao, John Bocco, vijana wa Mcameroon, Joseph Omog wameshindwa kutamba mbele ya maafande, hivyo kujivunjia rekodi yao ya msimu uliopita, ambapo waliichapa Ruvu Shooting katika mechi zote.




No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...