Add caption |
Kiungo wa Schalke, Felix Platte (kushoto) na beki wa Real Madrid, Daniel Carvajal wakiwania mpira katika mchezo wa jana. |
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa), Real Madrid ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Schalke 04 usiku, umeifanya ifikishe idadi ya mechi, sawa na Bayern Munich kwa kushinda mechi 10 mfululizo, rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na mabingwa hao wa Ujerumani.
Mabao ya Cristiano Ronaldo na beki, Marcelo Vieira ugenini yaliifanya Real kuwa katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali katika mbio za kuutetea ubingwa wao.
Matajiri hao wa dunia, walitangulia mbele kwa bao la staa, Ronaldo (CR7), ambaye alimaliza ukame wa mabao baada ya kutofunga katika mechi tatu mfululizo kabla ya Marcelo kupigilia msumari wa mwisho.
Ushindi huo, uliwafanya vijana wa kocha Carlo Ancelotti kuifikia Bayern, katika michuano hii, baada ya Wajerumani hao kuandikisha rekodi hiyo Novemba 2013 baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi.
Madrid walianza kampeni hii msimu uliopita, baada ya kuivuruga Bayern katika hatua ya nusu fainali kabla ya kutwaa ubingwa mbele ya Atletico Madrid. Mbio zao ziliendelea tena msimu huu hatua ya makundi baada ya kushinda mechi zote ikiwa ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza pointi hata moja mpaka sasa kwenye hatua ya 16.
Mabingwa hao maarufu kama ‘The Blancos’ wanatarajia kuvunja rekodi hiyo iwapo tu wataifunga tena Schalke 04 katika mechi ya marudiano kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.

CR7 akifunga bao lake la 76 na kuwafikia Messi na Raul katika ufungaji bora wa mabao Ulaya. Pia lilikuwa bao lake la 12 mfululizo kufunga katika mechi za ugenini kwenye michuano hii. |
No comments:
Post a Comment