Moja ya picha ikimuonyesha Kissu akiwa kwenye majukumu ya utangazaji TBC Taifa |
Katika kile kinachoonekana sekta ya soka inazidi kupaa zaidia hapa nchini, Rais, Jakaya Kikwete amewateua magwiji wa soka hapa nchini, Fredrik Mwakalebela pamoja na Shaban Kissu kuwa wakuu wa wilaya, katika uteuzi uliofanywa juzi na rais huyo.
Mwakalebela ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amepata ulaji mpya kama mkuu wa Wilaya ya Wang’ing’ombe huko mkoani Njombe huku Kissu ambaye ni mwanahabari aliyebobea katika kutangaza michezo TBC 1 na TBC Taifa, akila ‘bata’ katika Wilaya ya Kondoa, huko Dodoma.
Mwakalebela ambaye ni katibu wa kwanza katika utawala wa rais, Leodegar Tenga, amesema amefurahishwa na uteuzi huo na mbali ya kwenda kuwatumikia wananchi wa Wang’ing’ombe pia anataka kwenda kuhakikisha anatumia uzoefu wake wa michezo kuipaisha wilaya hiyo.
Mwakalebela alisema baada ya kufika eneo hilo atafanya ziara ya kutaka kujua matatizo ya msingi na kuyatafutia ufumbuzi. Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya kwa kuwateua wapya 27, kuwahamisha 64 na wengine 42 amewabakiza kwenye vituo vyao.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na vifo vya wakuu wa wilaya watatu na mabadiliko mengine ikiwamo kupandishwa vyeo.
KWA HISANI YA MWANASPOTI

No comments:
Post a Comment