Kiungo wa Ruvu Shooting, Juma Nade kushoto akijaribu kumtoka Hamis Mcha wa Azam katika mchezo wa mwisho timu hizo zilizopokutana msimu jana. |
Jerry Tegete akikwamia mpira katika moja ya mchezo na Prisons, chini ni aliyekuwa kipa wa Prison, David Burhan ambaye kwa sasa yupo Mbeya City. |
Azam ndio wapo kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, wakiwa na pointi 25, sawa na Wanajangwani, ambapo kocha wa Azam, Mcameroon anasema akili yao yote ipo kwa Al Merrikh katika mchezo wa marudiano kwenye michuano ya Ligi ya Mataifa Afrika.
Azam wanawakabili wanajeshi wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mlandizi, Pwani, huku Yanga wao wakiwa na kibarua cha aina yake kwenye Dimba la Sokoine, Mbeya kumeanyana na Tanzania Prisons.
Ikumbukwe kuwa Yanga haina rekodi nzuri kwenye uwanja huo, baada ya msimu uliopita kutoka na pointi mbili kati ya sita, jambo ambalo wataingia wakifahamu na kusaka ushindi wa lazima ili kufuta uteja.
Azam wao wamekuwa na bahati na Ruvu, ambapo msimu uliopita kuichapa ‘home and away’, lakini wanaweza kukumbana na upinzani wa hali ya juu, kufuatia Ruvu kuamua kuiendea Morogoro kuitafutia stamina ufukweni tangu Jumatatu.
No comments:
Post a Comment