Thursday, February 19, 2015

SNURA ANG'AKA KUAMBIWA ANA MTOTO MCHANGA



Msanii anayefanya muziki na filamu Bongo, Snura Mushi ameeleza kushangazwa kwake na taarifa zinazozidi kuenea kuwa amejifungua, jambo ambalo anadai eti siyo kweli. Madai ya staa huyo kujifungua kwa siri yameenea na hata wasanii wenzake wanajua hivyo lakini mwenyewe amekuwa akikanusha na kuwaacha mashabiki wake njia panda.Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni, Snura alisema yeye ana mtoto mmoja mkubwa lakini madai ya kwamba amejifungua hivi karibu hayana ukweli. “Mimi sina mtoto mdogo, mwanangu ni yule mnayemjua, hao wanaosema nimezaa mbona wananizalisha?” alihoji Snura ambaye baada ya muda mrefu kupotea, juzikati aliibukia kwenye Ukumbi wa Escape One ulipo Msasani, jijini Dar


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...