Mkuu wa Idara ya Habari wa Yanga (katikati), Jerry Murro akisitiza jambo katika mkutano na wanahabari leo kwenye Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani. |
Ngassa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akifafanua kuhusu deni linalomtesa. Kushoto ni mkuu wa idara ya habari, Jerry Murro.
Yanga imesema ipo tayari kusimamia deni la zaidi ya milioni
40 anazodaiwa na Benki ya CRDB alilokopa kwa ajili ya kulipa faini aliyopigwa
na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kusaini mkataba katika klabuni
mbili; Simba na Yanga ambapo alitakiwa kuilipa Simba, lakini ikasema kuwa
lazima kutakuwa na masharti ya kufuata ili kuhakikisha kiasi hicho anakirejesha.
Deni hilo limemtesa sana mchezaji huyo na kumtoa kwenye mudi
ya kucheza soka, kutokana na benki kumkata mamilioni ya fedha huku hivi karibuni
ikizuia mishahara yake miwili, jambo lililomfanya akose amani ndani ya klabu.
Akizungumza leo kwenye mkutano na wanahabari, Ngassa alisema
kuwa kutokana na deni hilo ameamua kuuomba uongozi kumsaidia kulipa deni hilo,
ambapo mkuu wa idara ya habari wa klabu hiyo, Jerry Murro
akikiri kumsaidia ndani ya wiki moja.
akikiri kumsaidia ndani ya wiki moja.
"Kama uongozi kwa kutambua umuhimu wa Ngassa kama mchezaji
wetu, tumeamua kuwa sekretarieti itakaa kuzungumzia ombi lake la kuomba
kumsaidia, naahidi tutamsaidia na ndani ya wiki moja suala hilo litakuwa
limetafutiwa ufumbuzi. Lakini ikumbukwe kuwa hela yoyote ile ya Yana ni mali ya
wananchi, hivyo ni lazima ziwe na utaratibu katika matumizi, vinginevyo
tutapigwa mawe. Kwa hiyo tunaahidi kumsaidia lakini tutaangalia ni jinsi gani
ya kuweza kurudisha kiasi hicho,” alisema Murro.
Kwa upande wa Ngassa, alifunguka kilichomnyima furaha klabuni
hapo ambapo alisema: “Ni kweli nikosa raha kutokana na makato makubwa kwenye
deni hilo. Nilikuwa nikikatwa kiasi fulani (laki tano) kwa kila mshahara,
lakini mshahara wangu wa miezi miwili sikuiona, iliniuma sana, hivyo nimewaomba
viongozi wangu kunisaidia katika hili, na wameniahidi kulifanyia kazi.
“Naamini litakwisha na nitarudi katika kiwango changu na nina
uhakika ninaweza kuwa haa mfungaji bora kama nilivyofanya msimu ulioisha
nilivyokuwa mfungaji bora wa Afrika kwenye michuano ya Shirikisho na mfungaji
bora wa klabu,” alisema nyota huyo wa zamani wa Simba, Kagera na Azam.
No comments:
Post a Comment