Kiungo mshambuliaji wa Yanga, amekata mzizi wa fitina baada
ya kusema kuwa hana matarajio ya kusaini mkataba mwingine katika klabu za
Tanzania badala yake anataka kucheza soka la nje iwapo mkataba wake utakwisha
mwishoni mwa msimu huu.
Ngassa mkataba wake umebakiza miezi mitano kumalizika, ambapo
bado hajasaini na amesema kuwa ndoto zake ni kucheza kimataifa zaidi na kwamba
katu hawezi kusaini katika klabu za hapa. Hata hivyo uongozi wa Yanga kupitia
kwa Mkuu wa Idara ya Habari wa Yanga, Jerry Murro ulisema hawapo
tayari
kumuachia kutokana na umuhimu wake klabuni hapo kwa sasa.
“Bado nina mkataba na Yanga na nitaendelea kuitumikia, lakini
Inshallah sitasaini tena timu za hapa, nitaangalia mbele zaidi,” alisema Ngassa
katika mkutano wa waandishi wa habari.
Kauli yake, inaaksi taarifa za kwamba nyota huyo alikuja
kuaaga mashabiki wa Yanga baada ya kuifungia
timu yake mabao mawili ya ushindi kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar Jumapili
na kuiwezesha timu hiyo kukaa kileleni kwa pointi 25, tatu zaidi ya Azam.
Ngassa mwenye jezi ya kijani, akidhibitiwa vilivyo na aliyekuwa beki wa Manchester United, Fabio Da Silva wakati akiwa na kikosi cha Seatle Sounders ya Marekani mwaka 2012. |
Taarifa zaidi zinasema kuwa nyota huyo ana dili la kujiunga
na klabu ya El Merreikh ya Sudan na ndiyo maana hataki kuingeza mkataba licha
ya uongozi wa klabu hiyo kutangaza kutaka kuanza mchakato wa kumuongezea
mwingine pamoja na wachezaji wengine wanaomaliza mikataba mwishoni mwa msimu
huu.
No comments:
Post a Comment