Murro akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari, hawapo pichani. |
Kwa wale wapenda vya dezo, sasa imekula kwao baada ya uongozi
wa Yanga kutangaza kuwa hautaruhusu mchezo wao wa kimataifa, dhidi ya DBF XI ya
Botswana kurushwa na kituo chochote,
lakini ukafafanua kuwa iwapo kampuni yoyote itajitokeza kuchangamkia
tenda hiyo kabla ya mchezo, basi wakazi wa Dar
watafaidi, vinginevyo wakaisikilizia kwenye bomba.
Jerry Murro ambaye ni mkuu wa kitengo cha habari, amesema kuwa
wamefikia uamuzi ya kupiga stop kuoneshwa kwa mchezo huo kwa kutaka wakazi wa
Dar kujitokeza kwa wingi siku hiyo, ikiwa ni moja ya kuipiga sapoti timu yao. Viingilio
vya mchezo huo vitakuwa ni
kuanzia buku tano (5,000) hadi 30,000 kwa kiingilio
cha juu na tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo.
Alikwenda mbali na kusema kuwa wapo tayari kuwasaidia wakazi
wa mikoani ambao si rahisi kuja uwanjani, lakini si kwa wakazi wa jiji kufaidi
uhondo wa bure.
“Wakazi wa Jiji la Dar mtatusamehe, tumepanga kutorusha
mchezo wetu moja kwa moja, na ni bora tukaruhusu ‘signal’ kurushwa mikoani
ambao tuna uhakika kuwa hawawezi kufika uwanjani. Tumeamua kuweka kiasi cha
chini ambacho tunaamini mtu yeyote anaweza kumudu akiamua, ndiyo maana tunataka
watu wajitokeze kwa wingi ili waisaidie timu kwa namna moja ama nyingine.
“Lakini iwapo kampuni itajitokeza kununua haki ya matangazo,
sisi tunawakaribisha ili tufanye biashara lakini iwe ni hela ambayo tunaamini itaisaidia
timu,” alisema Murro.
No comments:
Post a Comment