Tuesday, February 10, 2015

KISIGA AMUIBUKIA KOPUNOVIC MAZOEZINI, BENCHI ZIMA LAMVAA...CHEKI PICHA

Kocha wa Simba, Goran Kopunovic kulia akizungumza na Kisiga leo baada ya kiungo huyo kutokea mazoezini kwa mara ya kwanza tangu asusie na kuondoka kambini bila taarifa.





Kiungo aliyesusia na kutangaza kuwa hayupo  tayari kurejea kikosini hapo kwa sababu ambazo hakuzitaja, leo amewaibukia wachezaji wenzake katika mazoezi ya  klabu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mbweni Jeshini ambapo timu hiyo inajifua na mchezo wa Ligi Kuu Bara, dhidi ya Polisi Moro ukaopigwa Jumamosi hii.
 Kisiga aliondoka kambini tangu Jumatano iliyopita, baada ya kipigo cha mabao 2-1 walichopokea Simba kutoka kwa Mbey City.
Hata hivyo kocha, Goran Kopunovic amekuwa akisisitiza kutaka kukutana na mchezaji huyo kwani hajajua kilichomuondoa kikosin, ambapo wawili hao wamekutana leo na kuzungumza mambo kadhaa wakiwa 'chemba' kabla kukutanishwa na benchi zima la ufundi, pamoja na kocha msaidizi, Selemani Matola daktari wa timu, Yassin Gembe na coodnator wa timu.
Benchi zima la ufundi la Simba, Matola, daktari Gembe wakizungumza na Kisiga huku Kopunovic akiongeza coodinator.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...