PREZIDAA wa Bendi ya Malaika Music, Christian Bella 'King of the Best
Melodies' amewaahidi shoo kali mashabiki wake watakaohudhuria katika
Ukumbi wa Kisasa wa Dar Live, Jumamosi ijayo ambayo ni Siku ya
Wapendanao 'Valentine's Day'.
Staa huyo ameyasema hayo hivi punde wakati wa mkutano na wanahabari
wa vyombo mbalimbali uliofanyika katika ofisi za Global Publishers.
Bella amesema atakuwepo ndani ya kiwanja hicho mapema kuanzia saa 7
mchana na atapiga picha za red carpet na mashabiki wake watakaohudhuria
sambamba na kuzungumza nao mawili-matatu.
Mbali na kuwahi ukumbini, Bella amewaandalia nyimbo zake zote kali za
mapenzi kama vile Msaliti, Safari Siyo Kifo, Nakuhitaji pamoja na wimbo
bora uliofunga mwaka wa Nani Kama Mama.
Kuonyesha kuwa utakuwa Usiku wa Wapendanao, Bella amewaandalia
mashabiki wake zawadi ya wimbo mpya uitwao NASHINDWA ambao atauchia kwa
mara ya kwanza huku video akienda kuifanyia nchini Afrika Kusini wiki
ijayo.
Mbali na Bella usiku huo ambao ni maalum kwa wapendanao, mkali wa
muziki wa Mwambao, Mfalme Mzee Yusuf naye atakuwepo katika kuwaburudisha
mashabiki wote watakaokuwepo ukumbini hapo.
Usiku huo Mzee Yusuf atashuka na kundi lake la Jahazi Modern Taarab
na kuangusha ngoma zake zote kali za mapenzi kama vile My Valentine,
Wapendanao, Tiba ya Mapenzi, Wasiwasi Wako pamoja na hii ambayo ni
habari ya mjini kwa sasa ya Mahaba Niue
Christian Bella (kulia) akijibu baadhi ya maswali ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya shoo yake ya Valentine kwenye Ukumbi wa Dar LiveBella akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani).
Christian Bella (kulia) akiwapa vionjo vya wimbo wake mpya wa 'NASHINDWA' wanahabari (hawapo pichani). Kushoto ni mmoja wa viongozi wa Malaika Band, X-Bass Babu Bomba.
Bella akiwa na Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist X-Bass Babu Bomba na Bella katika pozi na Mpiga Picha wa GPL, Musa Mateja.
X-Bass Babu Bomba na Bella wakiwa katika picha ya pamoja na Mhariri Mwandamizi wa GPL, Walusanga Ndaki.
X-Bass Babu Bomba na Bella wakipozi na Shafii Mohamed wa GPL.
X-Bass Babu Bomba na Christian Bella katika pozi ndani ya GPL.

No comments:
Post a Comment