Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania, Yanga, wamezidi kuuonyesha umma kuwa si mabingwa wa heshima kwa kubahatisha, baada ya leo kuendeleza wimbi la ushindi, kwa kuibabua Mbeya City mabao 3-1.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Dimba la Sokoine, Mbeya, mabao ya Yanga yaliwekwa kimiani na Simon Msuva, Mrisho Ngassa kabla ya Amissi Tambwe kupigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la wenyeji. Peter Mapunda aliifungia City bao la kufutia machozi.
Kwa ushindi huo, Yanga imeendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 31.
Historia mpya Sokoine
Kikosi cha Yanga, chini ya Hans van Der Pluijm kinaweka rekodi ya aina yake, kwa kuondoka mkoani Mbeya kwa kuzoa pointi sita na mabao sita katika michezo miwili, kufuatia juzi Alhamisi kuichapa Prisons mabao 3-0. Hii inakuwa wiki ya rekodi kwa Yanga, kwani kabla ya hapo mara ya mwisho kuvuna ushindi uwanjani hapo ilikuwa ni mwaka 2009, walipoichapa Prisons bao 1-0 lililofungwa na Athuman Idd ‘Chuji’ ambaye kwa sasa ni nahodha wa Mwadui FC ya Shinyanga.
Tambwe aendeleza rekodi yake

Bao la Mrundi, ambaye ni nyota wa zamani wa Vital’O na Simba, Amisi Tambwe limemfanya kufikisha jumla ya mabao matano msimu huu, lakini rekodi ya aina yake ni kwamba yote ameyafunga kwa kichwa. Bao katika mchezo wa leo, aliunganisha kwa kichwa kona ya Haruna Niyonzima.
Rekodi ya Barthez kwishineyi!
Mlinda mlango kiwango kwa sasa, Ally Mustafa ‘Bartez’ kwa mara ya kwanza , leo ameruhusu bao, baada ya kukaa langoni mwa kikosi hicho dakika 560, sawa na mechi sita bila kuruhusu bao.
No comments:
Post a Comment