Sunday, February 22, 2015

KAANEEEEE....AIOKOA SPURS SEKUNDE MOJA YA MWISHO



Kane akiitoa kwenye mdomo wa mamba Spurs.... Akimalizia mpira wa penalti uliotemwa na kipa wa West Ham

Straika kiwango kwa sasa, Harry Kane ameendelea kufanya yake Ligi Kuu England, baada ya leo kuikoa timu yake ya Tottenham Hotspur, mbele ya West Ham, sekunde moja kabla ya kumalizika kwa mchezo.
Katika mchezo huo , Wagonga Nyundo wa London, West Ham, waliongoza kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 80 kwa mabao ya Cheikhou Koyoute na Diafra Sakho, lakini Spurs ikacharuka na kurudisha mabao yote, japo haikuwa kazi rahisi kutokana na kuonekana kuzidiwa soka kwa asilimia kubwa.
Danny Rose alipatia Spurs la kwanza dakika ya 81 akiunganisha kwa mkwaju mkali, mpira uliokuwa umeokolewa langoni mwa West Ham, kabla ya Kane kufanya yake dakika ya 86 kabisa sekunde kabla ya kipenga cha mwisho kwa mkwaju wa penalti.
Lawama zote za West zitamwendea Alex Song kwa kosa la kumfanyia madhambi Kane kwenye box katika dakika ya mwisho. Kipa wa West Ham alipangua penalti hiyo kabla ya Kane kuukwamisha tena wavuni.
Sare hiyo imeisaidia Spurs kufikisha pointi 44, katika nafasi ya sita huku West wao wakibaki katika nafasi ya nane na pointi 39, ikiwa ni sare yao ya tatu mfululizo.  
Bao la Kane linamfanya afikishe mabao 14, matatu nyuma ya Diego Costa wa Chelsea na Sergio Aguero wa Man City wanaokabana kileleni.

Bao la Kouyate wa West Ham

Bao la Danny Rose wa Spurs

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...