Marehemu, Alex Masawe wa tatu kutoka kulia waliosimama mwenye rasta akiwa na kikosi cha Simba. |
Aliyekuwa kiungo nyota wa Simba, Christopher Alex Massawe, amefariki dunia leo asubuhi huko mkoani Dodoma, baada ya kuugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na Ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB).
Dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Mama Maembe amesema Alex amefariki dunia leo saa 3 asubuhi katika Hospitali ya Mirembe.
Tayari taratibu za mazishi zimeanza kufanywa na imeelezwa marehemu atazikwa mjini humo.

CV YAKE
Marehemu, alizaliwa Septemba 12 mwaka 1975, alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Uhuru na kumaliza katika Shule ya Chamwino huko Dodoma mwaka 1993. Alianza kucheza soka kwenye kikosi cha Chamwino United katika timu ya daraja la nne na baadaye daraja la tatu akiwa na Aston Villa, nayo ya Dodoma.
Mwaka 1999-2001 aliitumikia klabu ya CDA ya Dodoma kabla ya kutimkia Reli ya Morogoro mwaka 2002 na baadaye kujiunga na Wekundu wa Msimbazi, Simba,
Kiungo huyo alijulikana kwa ubora wake katika ukabaji na kuichezesha timu, pia atakumbukwa kwa kuwa mchezaji aliyepiga penalti ya mwisho iliyoivua ubingwa Zamalek ya Misri na kuipeleka Simba kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika 2003.
Marehemu ameacha mtoto mmoja wa kiume aitwaye Alex.

Alex, enzi za uhai wake. |
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihidimiwe.
No comments:
Post a Comment