Kikosi cha Kagera Sugar |
Kikosi cha Kagera Sugar kimeendeleza wimbi la ushindi, ukiwa ni mchezo wao wa tatu mfululizo kupata ushindi wa bao 1-0, kufuatia leo kuicharaza Polisi Moro idadi hiyo ya mabao katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga jioni hii.
Bao pekee la straika aliye kwenye kiwango, Rashid Mandawa dakika ya 34, liliitosha Kagera kuondoka na pointi zote hivyo kufikisha pointi 24 katika nafasi ya tatu, mbili nyuma ya Azam na nne nyuma ya vinara Yanga ambao watashuka dimbani kesho kumenyana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya.
Azam kamali yao ya kuongoza pengo na Kagera itakuwa ni kesho wakati wakiwakaribisha vibonde wa ligi, Prisons kwenye Uwanja wa Chamazi , mchezo utakapigwa majira ya saa mbili usiku.
Mkoani Mtwara, Ndanda wamerejesha matumaini, baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal.
Mtibwa huruma tupu
Mtibwa Sugar imeendelea na wimbi baya la kupoteza, baada ya leo kuchezea kichapo tena mbele ya Mgambo Shooting, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga. Kichapo hicho ni nne mfululizo kwenye ligi kuu.
No comments:
Post a Comment