Saturday, February 21, 2015

TFF YAMPELEKA CHUJI AZAM

Mwadui FC
 
African Sports.
Fainali ya kumsaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), kati ya kinara wa Kundi A, Mwadui FC na vinara wa Kundi B, African Sports inatarajiwa kupigwa kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi kuanzia majira ya saa 10 jioni.
Awali mchezo huo ulikuwa umepangwa kufanyika kesho kwenye Dimba la Taifa, lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TTF, zimepelekea mchezo huo kuhamishiwa Chamazi ambao ni Uwanja wa Azam FC.
Mwadui iliyo chini ya kocha mwenye mbwembwe nyingi, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ikiwa chini ya nahodha wake, Athuman Idd Chuji, pamoja na mastaa kibao waliowahi kutikisa kwenye ligi kuu, itakutana na mahasimu wa kudumu wa Coastal Union ya Tanga, ambao pia wana wachezaji wakongwe, wakiongozwa na straika wa zamani wa Simba, Ally Shiboli pamoja na kipa wa Yanga, Yusuf Abdul.
Mchezo huo utaonyeshwa moja kwa moja na Azam TV ili kuwapa nafasi wapenzi na wadau wa soka waliopo mbali na hasa mikoani kuweza kushuhudia mchezo huo.
Bingwa wa Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza atazawadiwa Kombe pamoja na medali, huku mshindi wa pili akipata kikombe na medali pia.
Viingilio vya mchezo huo ni tsh.5,000 kwa jukwaa kuu na Tsh. 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...