Saturday, February 21, 2015

PAMBANO LA KARNE… MAN MONEY vs PACQUIAO TAMBO ZAZIDI KUMIMINIKA



Wanaume wa kazi... Picha zilizounganishwa zikiwaonesha wababe wa dunia kwenye ngumi kwa sasa, Man Pac kulia na Mann Money wanaotarajia kumaliza ubishi wao Mei mwaka huu.

Baada ya tambo za miaka mingi, hatimaye wafalme wawili wa ngumi duniani, Floyd Mayweather ‘Manny Money’ na Emmanuel ‘Manny’ Pacquiao, wamekubali kukata mzizi wa fitna na kuamua kukubaliana kupanda uliongoni mwezi Mei, 2 mwaka huu, pambano la kihistoria litakalowaingizia mamilioni ya fedha magwiji hao.
Pambano hilo litapigwa huko Las Vegas Marekani.

Mayweather raia wa Marekani ana umri wa miaka 37 na Pacquiao Mfilipino ana 36, kwa sasa ndio wanatajwa kuwa mastaa wa ngumi duniani katika kizazi cha sasa.

Wawili hao wamekuwa na tambo za muda mrefu huku mipango ya kukutana ili kukata mzizi wa

fitina kwa kumaliza ubishi wao imekwama mara kadhaa, lakini hatimaye muafaka umefikiwa na mbabe wa dunia atajulikana Mei kwa dau la hali ya juu zaidi, dola milioni 250 kila mtu.
Cha kuvutia zaidi ni wawili hao kutofautiana kimapambano, wakati Manny Money akishikiria mikanda mbali ya dunia ya WBC na WBA Welterweight, Pacq anao ubingwa wa mkanda wa dunia wa WBO welterweight.
Manny Money anashikiria rekodi ya kushinda mapambano yake yote katika mapambano 47 ya kimataifa aliyopanda ulingoni huku mpinzani wake kutoka Asia akiwa na ushindi wa mapambano 57, sare mawili na kupoteza matano katika jumla ya mapambano 64 aliyoshiriki mpaka sasa.

Pambano la Mei litakuwa la kihistoria katika mapambano ya ngumi karne hii, kutokana na kila bondia kujiingizia kitita cha dola 250 sawa na pauni Mil.162. Kitita hicho kinavunja rekodi ya lile pambano la Mann Money na Saul Alvarez la mwaka juzi, 2013, ambapo liliingiza kitita cha pauni Mil. 97.
Baada ya makubaliano ya pande mbili, Mann Money alitupia ujumbe kwenye tovuti yake: “Kilichokuwa kikisubiriwa na Ulimwengu hatimaye kimefika. Dili la Mayweather vs Pacquiao limefikiwa, sasa kukutana Mei 2, 2015.
"Litakuwa ni tukio kubwa na la kihistoria katika michezo. Mashabiki wa mchezo wa ngumi na michezo mingine duniani kote watashuhudia makubwa siku hiyo."
Man Pac amesema: "Nimefurahi kuwa na pambano na Floyd Mayweather na sasa ninaweza kuwapa mashabiki wangu mchezo waliousubiri kwa hamu kubwa miaka mingi. Wamesubiria kwa muda mrefu aina ya pambano hili kweli wanastahili. Ni heshima kubwa kuwa katika moja ya tukio la kihistoria kama hili.
"Ninapenda kutoa pambano hili kwa mashabiki wangu wote ambao walitamani liwepo na, ni kipindi cha kurudisha heshima nyumbani na Wafilipino wote duniani kote."
Mayweather Manny Money yeye anasema: "Kuwapa mashabiki kile wanataka ndilo lengo langu kila siku.” Mimi ni bora kuliko na pambano hili itakuwa ni nafasi nyingine ya kuonyesha uwezo wangu na huwa ninafanya kile kilicho bora, ambacho ni ushindi.


REKODI ZAO   


Manny Money
Man Pac
Jina
Floyd Mayweather                  
            Manny Pacquiao
a.k.a
Money
Pac Man
Mahali pa kuzaliwa
Las Vegas, USA
General Santos City, Philippines
Kuzaliwa
24 Feb1977 (37)
17 Des1978 (36)
Urefu
5ft 8in
5ft 6in
Mapambano
47, shinda 47 (26 KOs) 
64, shinda 57 (38 KOs), poteza 5, sare 2
Mikanda anayoshirkiria
WBC & WBA welterweight, WBC light-middleweight
WBO welterweight


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...