Mjumbe
wa Chama cha Maalbino Tanzania, Sophia Mhando (katikati), akizungumza
kwa uchungu katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,
kuhusu vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa pamoja na maandamano hayo ya
amani ya kwenda Ikulu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Action on Disability
& Development (ADD), Mathew Kawongo na Ofisa Habari Mahusiano ya
Umma wa Chama cha Albino Tanzania Josephat Torner.
Ofisa
Habari Mahusiano ya Umma wa Chama cha Albino Tanzania Josephat Torner
(kushoto), akizungumza kuhusu maandamano hayo. Kulia ni Makamu
Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Gabriel Aluga na Mtunza
Hazina, Abdillah Omari.
Wanahabari na watu wenye ulemavu wa ngozi Albino wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
CHAMA cha Albino Tanzania kimeandaa maandamano ya
amani nchi nzima ikiwa ni njia mojawapo ya kulaani mauaji yanayoendelea
nchini pamoja na kumlilia Rais Jakaya Kikwete kwa kile kinachodaiwa
kushindwa kutokomeza mauaji ya albino.
Maandamano hayo yanayotarajiwa kufanyika tarehe 2/3/2015 ambapo
yataanzia ofisi za chama hicho zilizopo Ocean road kuelekea ikulu na
ikiwa ni maandamano ya tatu kufanyika tangu mwaka 2008, kipindi amabcho
mauaji ya watu wenye ualbino yalizuka na kuenea kwenye mikoa mbalimbali
nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa
Habari Mahusiano ya Umma wa chama hicho, Josephat Torner alitoa wito
kwa wazazi na mashirika ya umma na binafsi kuwaunga mkono katika
maandamano hayo ili kutokomeza suala zima la mauaji ya maalbino
yanayoendelea
"Zaidi ya watu 76 wameuwawa na majeruhi zaidi ya 56 na makaburi
18 kufukuliwa na watu kuachwa na ulemavu wa viungo 11 kati yao na
watoto", Torner alisema
Torner aliendelea kusema kuwa analiomba jeshi la polisi kutoa
kibali na ulinzi na kwamba hawapo tayari kuwa wakimbizi katika nchi yao.
Nae Mkurugenzi wa Action on Disability & Development (ADD),
Mathew Kawongo alisema kuwa atakuwa mstari wa mbele na kushirikiana nao
kuhakikisha suala zima la kutetea haki zao
"Aidha Kawongo alitoa wito kuwa waandishi wa habari kuwaanika
hadharani wale wote wanaofanya vitendo hivyo vya ukatili kwa albino
bila kujali vitisho.
Pia,Sophia Mhando mwanachama wa Umoja wa albino Tanzania aliwaomba
wazazi na jamii kwa ujumla kuwa na moyo wa huruma kwa kile kinachodaiwa
baadhi yao kuwa chanzo cha mauaji hayo, na pia watasubiri kwa muda wa
miezi mitatu mbali na hapo watakwenda Umoja wa mataifa kwa mashitaka
zaidi.
No comments:
Post a Comment