Sunday, February 22, 2015

SIMBA YAPIGWA KAMOJA TU SHY

Simba leo imetepeta baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa ‘Chama la Wana’ Stand United, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na Mnigeria, Absolume Chidiebele katika kipindi cha kwanza, huku wachezaji wawili wa Stand wakilimwa kadi nyekundu kwa matukio tofauti.
Kichapo cha Simba, kinaifanya kuendelea kubaki na pointi zake 20. Kwa matokeo hayo yanaifanya Simba kuwa mteja kwa Stand kwani katika mzunguko wa kwanza kutoka sare ya bao 1-1, Uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...