Kocha wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo 'Julio' akikenua baada ya timu yake kufanikiwa kutwaa ubingwa wa heshima wa Ligi Daraja la Kwanza leo kwenye Uwanja wa Chamazi, Azam. |
Timu ya Mwadui ya Shinyanga, jana Jumapili ilifanikiwa kuichapa African Sports ya Tanga kwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali ya kumsaka bingwa wa jumla wa Ligi Daraja la Kwanza uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar.
Fainali hiyo ilikuwa ikiwakutanisha vinara walioongoza makundi yao katika ligi hiyo iliyomalizika hivi karibuni ambapo Mwadui waliongoza Kundi B huku African Sports wakiibuka kinara wa Kundi A.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua kutokana na kila timu kutaka kudhihirisha ubora wake, ulishuhudiwa bao pekee la mchezo huo likifungwa kwa kichwa na straika wa Mwadui, Kelvin Sabato aliyeunganisha krosi ya Razack Khalfan.
Hadi mwisho wa mchezo huo, Mwadui iliibuka kidedea kwa bao hilo huku kocha wao, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ akisikitishwa na ushindi huo mdogo walioupata kwani walidhamiria kuwafunga wapinzani wao mabao 5-0.
Naye, Joseph Lazaro ambaye ndiye kocha wa African Sports alisema wanashukuru kupanda ligi kuu lakini matokeo ya kufungwa na Mwadui hayakuwa mazuri kwao ambapo alisisitiza kuwa bado ana kikosi bora.
Mwadui ambao ni washindi wamekabidhiwa kombe, medali na hundi ya shilingi milioni tatu huku washindi wa pili African Sports wamepewa medali pamoja na hundi ya shilingi milioni mbili.

Kiungo wa Mwadui, Julius Mrope mwenye jezi ya bluu akitokwa na mchezaji wa African Sports katika mchezo wa kusaka bingwa wa Daraja la Kwanza. |
No comments:
Post a Comment