Wema Sepetu akiwa kwenye pozi la mahaba na Ommy Dimpoz.
HABARI inayotamba mjini kwa sasa ni uhusiano mpya wa Madame wa Endless
Fame Wema Sepetu na Mmbongo Fleva Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, uliozuka kwa kasi
kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita huku penzi lao likijionyesha zahiri kuwa
hakuna siri tena.
Chanzo cha habari hii kilieleza kuwa
Wema na Ommy Dimpoz wamekuwa
wapenzi siku nyingi isipokuwa kulikuwa na siri ya ndani sana jambo ambalo hata
sasa wanaendelea kulifanya kama siri ili Dimpoz asije kutofautiana na ndugu
yake Diamond, ila ukweli ni kwamba safari yao ya South imewafanya kujiachia
kiasi cha kuvujisha hadi picha zao wakiwa kitandani na hiyo mimi naweza kusema
ni danganya toto tu wanayoifanya kwetu na wengine waone kama maigizo.
Ukweli wa mambo unaeleza kwamba ukaribu wao ni dalili za wazi kuwa
mastaa hao wana banjuka tena bila kificho, maana juzi kati picha
zilizodhihilisha ishu hiyo zilitapakaa wakiwa kwenye kitanda kimoja, na wengi
wasiojua ukweli watasema ni maigizo, ila wajuzi wa mambo wametonya kwamba
Dimpoz amekuwa akitoka na Wema kitambo tangu ile mara ya kwanza ambapo Wema
aliachana na Daiamond.
Tanzania One, baada ya kutonywa ishu hiyo bila kulemba lililazimika kumtafuta Ommy
Dimpoz ili aweze kujibu tuhuma hizo, alipopatikana bila kupiga kona alisema
kweli yupo na Wema muda mrefu na hasa ni watu wanao shibana kupita maelezo
ingawa watu wengi huwa hawajui kilichopo kati yao.
“Mimi na Wema ni damu damu kitambo kingi sana, so ukiniuliza kuhusu
kulala naye kitanda kimoja pia ntakwambia umechelewa kujua maana sijaanza leo,
hata kusafiri naye si mara ya kwanza so unachoona ni juu yako kutafuta majibu,
ila hii ni zamu yangu acha nitimize ndoto zangu za siku nyingi, na wanaosema acha
waseme wao mimi maisha yasonge na waniache project yangu iendelee,” alisema
Ommy Dimpoz.
Kwa uapande wa Wema baada ya kufikishiwa madai ya kubanjuka na
kuonekana picha wakiwa bed moja na mbongo fleva huyo, alisema kuwa haoni kipya
kinachoulizwa hapo maana kila mtu ana jicho lake na namna ya kutafakali na
kuweza kufafanua jinsi aonavyo, pia kuna usemi hua unasema kwamba, hujui kusoma
hata picha kuangalia? Naomba niachwe na mambo yangu mwenyewe maana kila kitu
naamua mwenyewe vilevile nafanya kwaajiri yangu na si mtu mwingine.
No comments:
Post a Comment