Friday, February 13, 2015

BREAKING NEWS YANGA YASITISHA MCHEZO WAO NA BDF RUNINGANI

Taarifa mbichi kabisa zilizotufikia ni kwamba klabu ya Yanga, imetangaza rasmi kuwa mchezo wao dhidi ya BDF XI utakaopigwa kesho Uwanja wa Taifa, hautoonyeshwa popote pale, hii ni baada ya tangazo la awali kuwa wangekaribisha kampuni yoyote kujitokeza kununua haki ya matangazo ya mchezo huo.
Mkuu wa Idara ya Habari, Jerry Murro ametoa kauli hiyo hivi punde na kuwatahadharisha wale wote waliokuwa na mawazo ya kuusubiria majumbani kwao ama kwenye vibanda, kuhakikisha wanaanza mckahato wa kununu tiketi, ambazo zinapatikana Max Malipo.
Ikumbukwe viingilio katika mchezo huo ni kuanzia 50,000 hadi 20,000 kama kiingilio cha juu.
Murro Jerry

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...