Kiungo wa Real Madrid Sami Khedira, amekuwa na maisha ya
kubahatisha kwa sasa, kutokana na kuandamwa majeraha ya mara kwa mara, ambapo
ameamua kurejea nchini kwao Ujerumani
ili kukutana na daktari anayemuamini zaidi, Dr. Müller-Wolfhart, ambaye
anafahamika kwa utaalamu wa juu katika maumivu ya misuli, lakini bahati mbaya
ni kwamba nyota huyo hataonekana uwanjani tena mwezi huu.
Nyota huyo wa zamani wa Bayern Munich aliondoka na kurudi
siku moja baada ya kuruhusiwa na timu ya madaktari ya Real Madrid, lakini
majibu aliyorejea nayo kutoka kwa daktari Müller-Wolfhart, ni kwamba anatakiwa
kupumzika si chini ya wiki mbili. Doktari huyo hivi karibuni ndiye alimtibu
Luka Modric- kiungo wa Madrid.
Khedira alipata jeraha dogo kwenye paja la mguu wa
kushoto katika mtanange wa mahasimu wa jiji, dhidi ya Atlético de Madrid wikiendi iliyopita.
No comments:
Post a Comment