Kikosi cha timu ya Big Bullet cha Malawi kiliwasili jana jioni Bongo
kwa ajili ya kuweka kambi ya siku moja, kikijiandaa na mchezo wa kimataifa dhidi
ya Komorozine ya Comoro, utakaopigwa keshokutwa Jumapili huko Comoro.
Kikosi hicho kimefanya mazoezi yake leo kwenye Uwanja wa
Karume, Ilala ambapo kitaondoka nchini kesho kuelekea Comoro kuwavaa
Komorozine, ambapo ni vibonde wa Yanga, baada ya msimu uliopita kuwanyuka jumla
ya mabao 12-2 katika mchezo wa raundi ya kwanza kwenye michuano ya shirikisho.
Mrisho Ngassa, kiungo wa Yanga aliibuka mfungaji bora, baada
ya kufunga mabao sita katika michezo miwili dhidi ya timu hiyo, kabla ya Yanga
kutupwa nje ya Waarabu wa Al Ahly ya Misri.
Aidha kwa upande wa Yanga ambao kesho watashuka dimbani kumenyana
na BDF XI ya Botswana, wamefanya mazoezi asubuhi ya kunyosha viungo huku jioni
ya leo wakipumzika, tayari kwa kuwavaa hao ‘Wakhoxa’ wa Botswana.
Mabingwa wa Tanzania, Azam wao watakuwa na kimbembe Jumapili
keshokutwa kuwakabiri El Merreikh ya Sudan, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa
Chamazi, Complex.
Azam na Yanga mechi zao za maruadiano itakuwa ni wiki mbili
baadaye. Tayari Yanga wao wametangaza siku ya kuondoka kuwafuata BDF kuwa
safari itakuwa ni Februari 25, siku mbili kabla ya mchezo, utakaopigwa mji mkuu
wa Botswana, Gabrone.
No comments:
Post a Comment