Wednesday, February 18, 2015

WANAKWAYA TANZANIA WADAIWA KUMTENGA ROSE MUHANDO


MAZITO tena! Kufuatia madai ya kuchoropoa mimba ya miezi saba kulikodaiwa kufanywa na mwimba Injili nyota Bongo, Rose Muhando, baadhi ya waimbaji wenzake wamesema hawawezi kuwa naye karibu tena katika huduma.

Mwimba Injili nyota Bongo, Rose Muhando.

Wakizunguza na Amani kwa nyakati tofauti, waimba Injili hao walioomba majina yao kupigwa ‘kufuli’ walisema, kama kweli Rose aliitoa mimba ile kwa makusudi basi wao hawana sababu ya kumfanya ni mtoa huduma mwenzao.

“Lakini inawezekana ile mimba ilitoka yenyewe maana pia inawezekana. Au madaktari walimshauri kutokana na matatizo ya kiafya. Tatizo tulishasikia mapema kwamba ana mpango wa kuitoa ndiyo maana tulipomwona hana mimba tena tukaamini ametoa kwa makusudi kabisa,” alisema mmoja wao.
Hata hivyo, Amani lilimtafuta moja kwa moja mwimba Injili staa, Bahati Bukuku na kumuuliza kuhusu kuwepo kwa madai ya kumtenga Rose.

“Mh! Mimi sifahamu, sijasikia. Unajua hayo ni mambo binafsi, sijui lolote,” alisema Bahati.
Amani pia liliongea na mwimba Injili, Jennifer Mgendi ambaye alisema: “Sijafuatilia kwa karibu habari za Rose, nasoma kwenye magazeti yenu tu. Hivi, kwani hali ikoje kwa sasa? Maana sijasoma magazeti siku nyingi kidogo.”

Amani likamtafuta Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania, Stela Joel ambapo alisema: “Sisi kama chama msimamo wetu ni kufanyia kazi madai ya waimba Injili kama kuna ushahidi wa kutosha tunachukua hatua. Hata Rose tunamchunguza kuhusu hayo madai.”
Kwa upande wake, Flora Mbasha alisema hajui lolote linaloendelea.

Kuanzia saa 8:57, juzi, Amani lilimpigia simu Rose akapokea na mambo yakawa hivi:
Amani: “Dada Rose mbona mpaka leo hujasema lolote kuhusu madai ya kutoa mimba?”
Rose: “Ah! Waache wanaopenda kusema mimi siwezi kusema lolote. Wao wanajua wanaweza kusema sana kuliko mimi, sasa waseme mpaka wechoke wenyewe.”

Amani: “Lakini pia kuna madai kwamba eti waimba Injili wenzako wamekutenga kwa sababu hujasema lolote kuhusu madai ya wewe kutoa mimba.”Rose: “Kwani walikuja kuniuliza, kama wangekuja kuniuliza hapo sawa. Lakini nani alinifuata kuniuliza kwamba mbona tunasikia hivi na hivi.”

Amani: “Kwani hakuna aliyekufuata kukuuliza?”
Rose: “Mimi sijaona mtu.”Amani: “Oke, kwa sasa hivi upo wapi? Dar, Dodoma?”
Rose: “Niko nyumbani (Dodoma) nimepumzika zangu tu

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...