Wednesday, February 18, 2015

KILICHOMFANYA DIMPOZ ARUDISHWE BONGO HIKI HAPA!!!

 HATIMAYE STAA wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz ametua nchini usiku wa kuamkia leo, baada ya kurudishwa na watu wa usalama wa raia wa nchini Marekani ambako alikuwa ameenda kwaajili ya kufanya shoo zake mbili.
Ommy amerejeshwa nchini baada ya kubainika hakuwa na kibali cha kufanya shoo nchini humo, hivyo shoo zake hizo zinatarajiwa kupangwa  muda mwingine tena atakapoenda kumalizia vimeo hivyo.
Akizungumza na mtandao huu alisema kwamba, ametua nchini usiku wa kuamkia leo ambapo amekutana na maneno kibao ambayo wengi wanazani karudishwa Bongo kwakuwa alihisiwa kuwa na vitu vibovu jambo ambalo si kweli kwani karudishwa baada ya kuchelewa kufika katika shoo yake ya kwanza hivyo shoo yake ya pili ikagundulika kuwa hana kibali.
"Kweli nimerudi usiku wa kuamkia leo, na nimekutana na maswali ya kila aina watu wakibishana wengine wakisema eti nimerudishwa kwakuwa nimekutwa na vitu ambavyo si halali jambo ambalo si kweli, ukweli ni kwamba nilichelewa kufika kwenye shoo yangu ya kwanza hivyo siku ikawa imepita hivyo shoo nyingine ikawa bado haijachukuliwa kibali chake, watu wa usalama pale airport baada ya kuchunguza na kukosa kibali changu cha shoo wakaniambie nirudi hadi siku nyingine taratibu zitakapofuatwa," alisema Ommy Dimpoz.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...