MSANII wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amedaiwa kumchukua mpenzi wa msanii wa filamu ambaye pia ni mpigapicha, Farid Jamal ‘Farid Uwezo’ aliyejulikana kwa jina moja la Vivian.
Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper.
Chanzo cha habari kililiambia gazeti hili kuwa, tangu Wolper awe karibu na Vivi, Farid amekuwa akiumia sana kwani amekuwa akikosa muda wa kujiachia naye.
“Yaani Wolper kampora Farid Vivi wake, sasa hivi jamaa ameamua kumuacha maana anaona mambo hayaendi sawa.
“Watu wanajiuliza, Wolper anampa nini Vivi? Ni ushosti wa kawaida tu au kuna kingine. Maana mtu huwezi kumuacha mpenzi wako kisa msichana mwenzako,” kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Farid na alipopatikana alisema ni kweli Vivi alikuwa mpenzi wake lakini Wolper kampora.
“Vivian alikuwa ni mpenzi wangu lakini baada ya kuwa na urafiki na Wolper alibadilika na kunikataa.
“Nilishindwa kujua sababu kutotaka kuwa na mimi kwa kuwa Wolper ni msichana mwenzake. Inaniuma sana kwani nilikuwa nampenda sana, hata hivyo siwezi kumrudia kwani atakuwa ameshaharibika kitabia,” alisema Farid.
Msanii wa filamu Bongo, Farid Jamal ‘Farid Uwezo’.
Alipotafutwa Wolper kuzungumzia madai hayo alisema, anashangazwa na taarifa hizo na anachokijua yeye ni kwamba Vivian ni rafiki yake Farid ni mtu wake.
“Kwanza Farid ni mtu wangu wa karibu sana ambaye sidhani kama anaweza kusema maneno hayo. Pili Vivian ni rafiki yagu wa kawaida, mimi nadhani kuna maadui zangu wanataka kunichafua,” alisema Wolper.
No comments:
Post a Comment