Wednesday, February 18, 2015

SOMA MAUZAUZA YALIYOSABABISHA KUVUNJIKA KWA NDOA YA JAY DEE & GARDNER

Gardner G Habash na Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jay D’ siku ya harusi yao.

BAADA ya wiki iliyopita aliyekuwa mke wa mtangazaji wa kituo cha radio cha EFM, Gardner G Habash, mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jay D’ kumwaga sababu za kuachana na mumewe huyo, mkali huyo wa kutangaza ameibuka na kusema amechukizwa na maneno yaliyotolewa na aliyekuwa mwandani wake huyo huku akidai anamuachia Mungu.

Ishu hiyo iliyopata nafasi kwenye vyombo mbalimbali vya habari, ilitokana na Jide kuwapa watu nafasi mashabiki wake kumuuliza maswali katika mtandao wa kijamii, ambapo asilimia kubwa walitaka kujua kama kweli ameachana na mume wake au la.

Magazeti Pendwa kutoka Global Publishers yakaamua kumtafuta Gardner ili aweke bayana juu ya suala la ndoa yao kutokana na mwanamuziki huyo kuweka wazi kwamba tayari ndoa yao ilikwishasambaratika.

“Alichokisema na ulichokisikia ndiyo ukweli wenyewe. Hakuna ndoa tena, tumekwishaachana na kila mmoja kuchukua kilicho chake. Ila kila kitu namwachia Mungu na wala sina kinyongo naye,” alisema Gardner.
...Wakiwa kwenye pozi.

Siku chache zilizopita mwanamuziki Jide alifunguka kwamba hakutaka tena kuendelea kuishi na mume wake kutokana na tabia mbaya alizokuwa nazo mwanamume huyo, hali iliyomfanya kuishi pasipo kuwa na furaha katika kipindi kirefu cha ndoa yao.
Akifunguka zaidi, Jide alisema kwamba alichoshwa na tabia hizo ambazo alipobanwa zaidi ili aziweke wazi tabia hizo, alisema kwamba mwanamume huyo alikuwa na tabia ya kuwashikashika wanawake kila alipokuwa jukwaani akiimba.
Alipenda kuwatongoza wanawake wengi tu ambapo kuna siku alimkuta akimshikashika mapaja mwanamke ndani ya mghahawa wake, na alipomuuliza, alikiri kufanya hivyo na kuomba msamaha.
Wawili hao walifunga ndoa Mei 14, 2005, jijini Dar es Salaam ambapo mpaka wanaachana, hawakubahatika kupata mtoto.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...