Wednesday, February 18, 2015

INGIA HAPA USOME JINSI WEMA SEPETU, KAJALA WALIVYO KINUKISHA KISA.....



HABARI ya mjini ni kwamba, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amedaiwa kumuumbua shosti wake wa zamani, Kajala Masanja kwa kumwaga ‘ubuyu’ kwamba amefilisika baada ya kigogo maarufu kama CK anayedaiwa kuwa ndiye mpenzi wake, kuyumba kiuchumi, Amani linakupa mchapo kamili.
Kigogo huyo aliyewahi kuwa na uhusiano na Wema kisha kumwagana naye, imedaiwa kuwa ile jeuri ya kununua magari ya kifahari, kumiliki biashara mbalimbali mjini, kwa sasa ameangukia pua kwani hawezi tena kujitutumua.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na Wema, baada ya kuhamishia majeshi kwa Kajala, Wema hakufurahia hivyo aliposikia uchumi umeyumba, amefurahia sana kufuatia ule msemo wa ‘adui muombee njaa.’
“Wema amefurahi sana, anawaambia marafiki zake kuwa malipo ni hapahapa duniani, Wema alimlipia Kajala dhamana ya sh mil. 13 ili asifungwe kwa msala wa kutakatisha fedha uliokuwa ukimkabili lakini akamgeuka na kumchukulia bwana wake, ule si ubinadamu kabisa,” kilisema chanzo hicho.
KAJALA ANA NUKSI?
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, Kajala ana nuksi kwani CK alipokuwa na Wema alikuwa na mafanikio na kupata fedha kila kukicha lakini alipohamia kwa Kajala mambo ndiyo yakaharibika.
“Kajala ana nuksi, CK alipokuwa na Wema walikuwa wanapata fedha nyingi kila wakati lakini kwa Kajala wamefilisika kwelikweli,” kilisema chanzo na kuongeza:
WEMA AMSHANGAA CK
“Madam mwenyewe amemshangaa sana CK kuishiwa fedha wakati alikuwa mtu wa kucheza na dola nyingi kila kukicha na aliwekeza fedha zake katika miradi mbalimbali.”
CK AMEPATWA NA NINI?
Jitihada za kumpata CK ili azungumzie ishu ya kuyumba kiuchumi hazikuzaa matunda lakini kwa mujibu wa mmoja wa watu ambao wanafanya naye kazi, kigogo huyo ameporomoka kiuchumi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kufanya magumashi ya fedha kazini hadi kufikia hatua ya kutaka kufukuzwa kazi.

“CK hayuko vizuri kazini, ana majanga kibao, ile jeuri aliyokuwa akifanya na Wema na Kajala ilikuwa ni fedha za magumashi sasa kimemnukia kazini,” kilisema chanzo hicho ingawa mwenyewe alipotafutwa kwenye simu hakupatikana.
MAZUNGUMZO YA WEMA YATHIBITISHA
Wakati mwanahabari wetu akiendelea kuichimba habari hiyo, alifanikiwa kunasa ‘clip’ ya sauti ya Wema iliyoonesha dhahiri kwamba mrembo huyo amefurahishwa na kitendo cha wawili hao kukalia kuti kavu.
Sauti hiyo ya Wema inasikika akizungumza na shosti yake kumueleza jinsi gani Kajala ameumbuka maana alifikiri kutembea na shemeji yake ameula kumbe matokeo yake ameangukia pua kwani mwanaume amefilisika.“…Kajala sasa hivi anaendesha Noah (Toyota) ile yenye mastikamastika nakwambia…” ilisikika sehemu ya clip hiyo.
WEMA ASAKWA
Paparazi wetu alimvutia waya Wema ili aweze kufunguka zaidi kuhusiana na sakata hilo namna ambavyo amefurahia, simu yake iliita bila kupokelewa.Hata hivyo, mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwake, mtaa wa Bwawani-Kijitonyama jijini Dar zaidi ya mara tatu kwa nyakati tofauti lakini hakufanikiwa kumpata baada ya mlinzi kudai amelala.
KAJALA ANASEMAJE?
Mwanahabari wetu alimvutia waya Kajala ili kusikia naye anasemaje baada ya kudaiwa kuanguka kiuchumi, simu yake iliita bila kupokelewa lakini hata hivyo, rafiki yake wa karibu ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alikanusha madai ya kufilisika.“Kajala hajafilisika na hawezi kufilisika, hayo yatakuwa maneno ya watu tu,” alisema rafiki huyo wa Kajala.
TUJIKUMBUSHE
Wema na Kajala waliwahi kuwa mashosti wa damu kabla ya kugombana ambapo chanzo kilitajwa kuwa ni CK,  mwaka jana walidaiwa kupatana lakini baadaye ikaelezwa kuwa bado wanaendeleza bifu

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...