Mnataka pointi ama show game?... Licha ya Man United kushinda lakini wengi wanaponda kiwango cha timu. |
Lakini pamoja na hayo, bado inaandamwa na lawama kutoka kwa mashabiki wake. Kila ushindi inaoupata, lazima uambatine na neno ‘lakini’. Hakuna ushindi wa timu hiyo chini ya Louis van Gaal unaweza kupita bila swali lolote.
Wiki iliyopita, United iliichapa Burnley lakini
ilionekana kuwa dhaifu na kucheza chini ya kiwango, hadi pale alipolazimika kubadili mfumo na kucheza 4-4-2 uliozoeleka kikosini hapo enzi wa Sir Alex Ferguson.
Wadau wanamuona Gaal kama yupo katika kategori ya waliofeli, wanaziona mbinu zake kama zimefeli. Iwapo United itamaliza katika nafasi za tatu za juu na kutwaa ubingwa wa FA, jambo ambalo wanaweza kutimiza, atakuwa amefanikiwa ‘tageti’ zake.
Kwa matokeo, United imefanikiwa kwa kiasi kikubwa, lakini mbinu za ushindi huo ndizo zinaleta ‘kasheshe’. United imekuwa na wachezaji hatari katika safu ushambuliaji, lakini kwa msimu huu si hatari tena na kwa mara moja moja kuonesha makeke, tofauti na misimu mingine.
Lile soka la kuvutia, kushambulia lililokuzwa na Sir Alex Ferguson, limeanza kufa na badala yake soka la nguvu limechukua nafasi.
Kwa muda mrefu, United imeonekana kuvutiwa na staili ya kuisogeza timu pinzani, badala ya kuwapa wakati mgumu- kuwabania juu kwa juu, jambo linalowakera mashabiki na kuibeza timu yao kwa jinsi wanavyotaka. Siku zote ni muumini wa mfumo wa 3-5-2 na hivi karibuni alisikika akisema katu hataki kuusikia mfumo wa 4-4-2 licha ya wengi kumtaka hivyo.
Punguza ubabe mdogo wangu... Sir Alex Ferguson kulia katika moja picha na Van Gaal. |
Katika mchezo na Burnley, United ilionekana bora hadi Van Gaal alivyolazimika kukubali kuibadili timu na kucheza mfumo ‘nuksi’ kwake, wa 4-4-2 baada ya kuumia kwa Daley Blind.
Na katika mchezo wa jana Jumatatu, walimiliki mpira kwa asilimia 71 hadi kipindi cha kwanza, lakini ajabu ni kwamba hawakuwa na shooti hata moja lililenga lango la Preston. Ni mpaka pake Ashley Young alipobadilika kipindi cha pili na kucheza soka la kupanua (width and pace), ndipo ikapata mabao.
Wapo mashabiki wanaofurahia timu timu kupata matokeo mazuri msimuu huu. Lakini wengine wanalia na aina ya uchezaji wa timu yenyewe, kwa kuiona kuwa ipo hatarini kupoteza kutokana na staili ya kuwaachia wapinzani kuwa huru (free-flowing) na kucheza sanasana soka la kuelea nyuma sana (swashbuckling football). Hapa ndipo anawapa nafasi ya kuchagua moja mashabiki wake, maana hawawezi kubeba yote kwa wakati mmoja.
Hatimaye van Gaal anatakiwa kufikisha yote- staili na matokeo, ndilo jambo mashabiki wanataka na si vinginevyo. Ndio uhondo waliouzoa enzi la babu Ferguson. Japo hawakuwa na matokeo mazuri wala soka la kuvutia katika utawala wa ‘anko’ David Moyes msimu uliopita.
Hivyo van Gaal hatakiwi kuingia katika kategori ya Moyes, anatakiwa kufanikisha walau mojawapo.
No comments:
Post a Comment