Bahanuzi kulia, katika uzi wa Polisi Moro. |
Usiyempenda kaja! Ndiyo kauli inayofaa kutumika kwa maajabu ya Said Bahanuzi wa Polisi Moro, mchezaji aliyekosa amani katika kikosi cha Yanga kwa muda mrefu huku akiandamwa na mashabiki, kisha kupelekwa kwa mkopo huko Polisi msimu huu, ajabu ni kwamba leo ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi wa ligi kuu.
Bahanuzi hakuwahi kukubalika kwa mashabiki wa Yanga pamoja na makocha waliopita, huku muda mwingi akikaa benchi, kama si kutoitwa kabisa katika kikosi cha wachezaji 18 kwenye mchezo husika.
Akizungumza leo katika mkutano wa waandishi wa habari, msemaji wa TFF, Baraka Kizuguto, alisema Bahanuzi amechaguliwa kama mchezaji bora wa mwezi Januari mwaka huu, huku tuzo ya mchezaji bora mwezi Desemba ikienda kwa John Mahundi wa Coastal Union.
Mahundi alitoa mchango mkubwa kwa timu yake ya Coastal Union Desemba mwaka jana na kuchaguliwa na jopo la makocha linalofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora wa kila mwezi kama ilivyo kwa Bahanuzi aliyeisaidia Polisi kupaa hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo kabla ya kushushwa wikiendi iliyopita.
Wawili hao watazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja kila mmoja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
Jopo maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.

Heshima pekee ya mchezaji huyo kwa Wanajangwani, ni kutwaa kiatu cha ufungaji bora wa michuano ya Kagame mwaka 2012 kwa kufunga mabao sita na kuisaidia Yanga kutwaa ubingwa huo.
Maisha yake Yanga, Bahanuzi (wa pili kutoka kulia, mwenye kiduku) akiwa benchi enzi akiwa Yanga. |
REKODI YA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI 2014/15:
Septemba- Anthony Matogolo (Mbeya City)
Oktoba- Salum Aboubakary 'Sure Boy' (Azam)
Novemba- Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
Desemba- John Mahundi (Coastal Union)
Januari- Said Bahanuzi (Polisi Moro)
No comments:
Post a Comment