Stori: Musa Mateja/Ijumaa
Sakata la kupangishiwa nyumba za kifahari na wanaume linazidi kuchukua
sura mpya kwa mastaa wa kike ndani ya tasnia ya sinema za Kibongo ambapo
safari hii mastaa wawili, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Jacqueline Walper
‘ Wolper’ Massawe wanadaiwa kuoneshana jeuri ya mabwana wakipima ni
yupi mwenye mshiko zaidi huku akina Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja
ambao awali walikuwa juu wakipotezwa.
TAMBO ZA NANI ZAIDI?
Uchunguzi wa Ijumaa
umebaini kwamba, kumekuwa na kasumba ya baadhi ya mastaa hao kutambiana
kuwa ni nani zaidi anayemiliki bwana mwenye mawe au mshiko kuliko
wengine.
Ilidaiwa kwamba, baada ya Lulu kuripotiwa kupangishiwa bonge la jumba
la kifahari na milionea maarufu wa jijini Arusha lililopo maeneo ya
Mbezi-Beach jijini Dar, Wolper naye anadaiwa kujibu mapigo kwa
kupangishiwa mjengo wa maana na bwana’ke uliopo maeneo hayohayo.
Kwa
mujibu wa vyanzo vyetu ambavyo ni watu wa karibu wa mastaa hao, kwa
sasa wawili hao ni moto wa kuotea mbali kwani kila mmoja amepata bwana
mwenye ‘mpunga’ mrefu.
WOTE WANALIPA SH. MIL. 30
Ilidaiwa kwamba, kama
ilivyokuwa kwa Lulu, Wolper naye analipiwa nyumba hiyo kiasi cha dola
za Kimarekani 1,500 kwa mwezi (zaidi ya Sh. milioni 2.4) karibia Sh.
milioni 30 kwa mwaka.
CHUMBA KAMA BOUTIQUE
Habari zilidai kwamba, kama
ilivyo ya Lulu, nyumba hiyo aliyopangishiwa Wolper ina vyumba kibao vya
kulala, ukumbi wa wageni, sehemu ya kulia chakula, mabafu, majiko n.k.
Pia nje ya nyumba hiyo kuna eneo kubwa la bustani iliyopambwa kwa maua mazuri na eneo la kutosha la maegesho ya magari.
Pamoja na kupangishiwa mijengo hiyo ya kifahari ushuani, Lulu na
Wolper wamekuwa wakioneshana jeuri ya magari waliyonunuliwa na
mabilionea hao.
MAGARI
Uchunguzi unaonesha kuwa Lulu ana mkoko
aina ya Toyota Rav4 New Model wenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni
30.Kwa upande wake Wolper anasukuma ndinga aina ya Toyota Prado, nalo
lina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 30.
WATOFAUTIANA VITU VICHACHE
Habari za ‘kiubuyu’
zinadai kwamba wawili hao wanapishana vitu vichache mno kama vile aina
ya mawigi na aina ya maisha (life style) ambapo bwana wa Wolper amempiga
‘stop’ kuigiza lakini bado Lulu anapiga mzigo.
“Lulu na Wolper wamelamba bingo za nguvu na bahati nzuri wanaonekana
wote kupata mabwana wasiokuwa na sifa.“Kwa mfano, Lulu pamoja na kuishi
katika maisha mazuri bado anasomeshwa na tayari ameshakamilishiwa ujenzi
wa nyumba yake ambayo juzikati alimkabidhi mama yake kama zawadi.
WOLPER AKOSWA, MAJIRANI WAFUNGUKA
Ijumaa
lilimtafuta Wolper kupitia simu yake ya mkononi lakini iliita bila
kupokelewa. Mwandishi wetu alifika mtaa anaoishi Wolper, akagonga sana
geti lakini halikufunguliwa.Hata hivyo, majirani wa staa huyo wamedai
kuwa amekuwa akionekana akiingia na kutoka akiwa ndani ya gari hilo aina
ya Toyota Prado. Jitihada za kumtafuta zinaendelea.
No comments:
Post a Comment