Saturday, February 14, 2015

SIKIA HII YA AZAM NA EL MERREIKH

Leonel Saint-Preux, straika wa zamani wa Azam katikati akipenya ngome ya El Merreikh katika michuano ya Kagema mwishoni mwa mwaka jana nchini Rwanda.

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Azam kesho watakuwa kwenye Uwanja wao wa  Chamazi Complex kumenyana na mabingwa wa Sudan, El Merreikh, ukiwa ni mchezo wenye angalizo kubwa sana.
Ni mchezo wenye taswira tofauti, ikiwa Azam wana uelewa mkubwa juu ya wapinzani wao kuliko El Merreikh wenyewe wanavyoifahamu Azam.
Licha ya kwamba mapema mwezi uliopita, mashushushu wa El Merreikh walikuja Tanzania kufuatilia nyendo za Azam kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, lakini si hoja ya msingi katika kuwakamata kwani Azam hutambulika kama moja ya timu yenye benchi kali la ufundi katika ligi kuu bara.

Ndondoo KUNTU  kuelekea mchezo wenyewe

. Azam ina faida ya kuwa na watu wengi wanaoifahamu El Merreikh, ambapo beki wao wa kutumainiwa, Serge Wawa raia wa Ivory Coast alitokea El msimu huu na kujiunga na Azam. Pia kocha msaidizi, Geroge Best Nsimbe msimu uliopita akiwa Kocha Mkuu wa KCCA ya Uganda, alikutana nao kwenye michuano kama hii, ambapo KCCA iliichabanga El mabao 2-0 katika mchezo wa awali, lakini wakapoteza kwenye mchezo wa marudiano.
. Mara ya mwisho wawili hawa kukutana ilikuwa mwaka jana katika michuano ya Kombe la Kagame huko Kigali, Rwanda katika hatua ya robo faianli, ambapo timu hizo zilitoshana nguvu lakini Azam wakaondolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-3.
. Mbali na kuwa mabingwa wetetezi pande zote, pia timu zote zipo kileleni katika ligi zao mpaka sasa. Azam wapo kileleni na pointi 25 sawa na Yanga lakini wapo juu kwa idadi ya mabao ya wastani, huku El Merreikh wao wakiwa kileleni kwenye ligi yao na pointi 10 katika mechi nne walizocheza. Wanafuatiwa kwa karibu na Al Hilal yenye point inane (8).

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...