Deogratius Munish 'Dida' anatadaiwa kuwa langoni leo, baada ya kumuachia lango Ally Mustafa 'Bartez' kwenye michezo ya ligi kuu hivi karibuni.
Walete hao Wamakonde wa Jeshi....Yanga katika tizi la mwishomwisho kwenye Uwanja wa Taifa. |
Kikosi cha BDF XI kikiwa mazoezini jana kwenye Uwanja wa Karume, Ilala kikijiandaa na mchezo wa leo dhidi ya Yanga. |
BDF |
Yanga
Baada ya maneno mengi kuzungumzwa takribani wiki tatu
zilizopita juu ya mchezo wa kimataifa wa Shirikisho Afrika baina ya Yanga na
BDF XI, hatimaye mwisho wa tambo umefika, ikiwa leo ni siku ya kuona kile
walichokuwa wakinadi Yanga na wapinzani wao.
Katika mkutano na waandishi wa habari jana, kuhusu mchezo
huo, Kocha wa BDF Meja, Letang Kgengwenyang alionekana kuinanga Yanga kwa
kusema kuwa anaifahamu kuwa ni timu ya soka la kujilinda zaidi ndiyo maana
inapata mabao machache katika mechi zake, huku pia akitoa tahadhari kwa Yanga
kuwa iwapo ‘watanengeneka’ na ‘home advantage’, wamekwisha!
Hakuna kuremba wewe...tuko fiti, Wazee wa kazi Yanga |
Wakinengeneka tu! Wamekwisha..BDF wakiendelea na tizi la tahadhari kubwa. |
“Hali ya hewa ya huku ina changamoto kubwa, kuna joto jingi,
lakini pia tutapambana kuhakikisha tunaizoea. Wakati nacheza niliwahi kukutana
na wachezaji wa Kitanzania na ninajua staili ya soka la hapa. Hata Yanga naijua
japo sio sana, zamani ilikuwa ikicheza soka la kushambulia kwa nguvu na muda
wote, tofauti na ya sasa-hii inacheza zaudi kujilinda,” alisema meja Letang.
Meja Letang. |
Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm alitoa tahadhari kwa
wachezaji wake kutodharau timu yoyote katika michuano mikubwa kama hii, hivyo
utakuwa ni mwendo wa kushambulia kama nyuki ili kujiweka katika mazingira
mazuri.
“Si mechi ya kubeza, tunatambua kuwa tunaingia uwanjani kama
wawakilishi wa taifa, hivyo ushindi wetu ni furaha kwa wote. Kwenye
michuano kama hii, hakuna timu ya
kuidharau ni kusaka ushindi kwa nguvu zote. Cha msingi mashabiki wajitokeze kwa
wingi kutupa sapoti,” alisema Pluijm.
Mchezo wa marudiano, utapigwa Februari 27 huko Gabrone,
Botswana.
No comments:
Post a Comment