Austin katikati akijaribu kuwatoka mabeki wa Southampton jana. |
Kifo kimezidi kuinyemelea klabu ya QPR kufuatia
nyota tegemeo katika harakati za kujinasua kushuka daraja, Charlie Austin na
Richard Dunne, kuripotiwa kuwa watakosa mechi zote zilizosalia msimu huu baada
ya kuumia katika mchezo wa jana dhidi ya Southampton.
Austin ndiye kila kitu pale Loftus, akiwa
ndiye kinara wa mabao wa timu kwa mabao
13 mpaka sasa, hata hivyo QPR kwa sasa inaanza mikakati wa kupata mbadala wake.
Dunne alijitonesha katika dakika ya 83 jana. |
Matumaini ya timu hiyo kubaki ligi kuu yamezidi
kunyongonyeshwa, huku jana ikikubali kichapo cha bao la usiku sana la Saido Mane
dakika ya 93, hali inayowafanya kubaki katika ukanda wa kushuka daraja.
Inaripotiwa kuwa kocha wa zamani wa Spurs,
Tim Sherwood anatajwa kuchukua mikoba ya kukinoa kikosi hicho, baada ya Harry
Redknapp kunyosha mikono mapema wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment