Manchester United imeponea chupuchupu kukumbana na kichapo
kutoka kwa Wagonga Nyundo wa London, West Ham United, baada ya kiungo Daley
Blind kuipatia bao la kusawazisha dakika za mwisho kabisa.
Wenyeji, West walitangaulia kupata bao dakika ya 49 kupitia
kwa Cheikhou Kouyate baada ya kutumia
vema uzembe wa mabeki wa United ambapo aliuchezea
mpira alivyotaka na kutumbukia nyavuni.
De Gea alikuwa nyota wa mchezo, akipangua moja ya michezo ya hatari kwenye mchezo huo. |
Amebana amechia...mpira uliopigwa na Kouyate (kushoto aliyeanguka chini) ukitinga wavuni huku kipa De Gea akiwa amepotea mabyoya. |
Mbali na bao hilo, jahazi laUnited lilionekana bayana kupwaya
kwa kipindi kirefu huku asimilia kubwa safu ya kiungo kuonekana kucheza chini
ya kiwango. Aidha shukurani zote, zitamwendea kipa wao, David De Gea ambaye
alifanya kazi kubwa kuokoa hatari nyingi langoni huku United wakifika aghalabu
langoni mwa West Ham.
United ilisawazisha bao hilo dakika ya 92 zikiwa zimebakia dakika
mbili katika zile za fidia kupitia kwa Blind. Hata hivyo Man wamepata pigo
baada ya beki wao, Luke Shaw kupewa kadi mbili za njano na kutolewa kwa kadi
nyekundu.
Blind (wa pili kulia) akiifungia United bao la kusawazisha, dakika mbili kabla ya kipyenga cha mwisho. |
Kipa wa WEst Ham akiruka bila mafanikio katika kuokoa shuti la Blind. |
NUKUU MUHIMU: Man United haijawahi kupata ushindi
katika mechi ilizosawazisha tangu Louis Van Gaal aanze kuifundisha timu hiyo.
Pia Man U haijawahi kushinda mchezo wowote kwa kutokea nyuma ikiwa kwenye
uwanja wa ugenini tangu Desemba 2013.
|
Katika mechi nyingine, sare iliendelea kutawala, baada ya
Newcastle United na Stoke City kutoshana nguvu ya bao 1-1 huku katika mchezo wa
awali, Bunley walitutumua na kuisimamisha West Brom kwa kufungana mabao 2-2.
No comments:
Post a Comment