MABINTI 22 wa Kihindi na Kinepal walioingizwa nchini kufanya biashara ya kuuza miili, wamenaswa wakimwaga machozi hadharani kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar wakisikitikia kuwakosa wateja wao Wabongo ambao inadaiwa walikuwa wakiwalipa vizuri. Mabinti hao waliingizwa nchini kati ya Mei na Desemba, mwaka jana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Dhamaka Entertainment Center Limited, Omprakash Singh kwa lengo la
kuwafanyisha biashara ya ngono katika klabu anazozimiliki.
Singh anadaiwa kuwa, alipowafikisha nchini makahaba hao, aliwapokonya hati zao za kusafiria kisha kuwafanyisha kazi hiyo pasipo kuwalipa mshahara ndipo Idara ya Uhamiaji nchini iliposimamia sakata hilo kwa kumshtaki mkurugenzi huyo mahakamani ambapo mahakama iliamuru makahaba hao walipwe mishahara yao na kurudishwa makwao.
Mapema wiki hii, chanzo makini kilimwaga ubuyu kuwa makahaba hao wanarejeshwa makwao, bila kuchelewa, mapaparazi wetu walitia timu katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere na kushuhudia makahaba hao wakifikishwa na gari la Uhamiaji lenye namba za usajili STK 9632. Baada ya kushuka, makahaba hao wakiwa katika sura ya huzuni, walisikika wakilia huku wakidai wanarudishwa nchini kwao ambako hawakuwa na kipato kikubwa kama walichokuwa wakipata Bongo.
“Kwa nini jamani wasituache wakati Bongo tumepazoea, tumetengeneza fedha nyingi wangetuacha tu kwanza tumeingia kihalali,” alisikika mmoja wa makahaba hao aliyezungumza kwa lugha ya Kiingereza.
Makahaba hao walikamilisha taratibu zote za kusafiri chini ya maofisa wa uhamiaji kisha wakaondoka na ndege ya Shirika la Qatar saa 12 jioni.Singh alitiwa hatiani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka baada ya kukiri kosa lililokuwa linamkabili la kuwaingiza nchini wasichana hao, ambapo aliwatumikisha kazi ngumu na biashara ya ukahaba kwa lengo la kujipatia fedha.
Mahakama ilimpa adhabu ya kulipa faini kila kosa Sh milioni tano hivyo kwa makosa matatu alitakiwa kulipa Sh milioni 15 na magari yake matatu yalitaifishwa na Serikali.Pia mahakama ilimtaka kuwalipa wasichana hao 22 mishahara yao na endapo mshtakiwa angeshindwa kulipa faini angekwenda jela miaka 10.
...Wakiwa na mizigo yao.
No comments:
Post a Comment