Thursday, February 12, 2015

BAADA YA KUPONDWA NA MITANDAO YA KIJAMII WAZIRI WA KILIMO,CHAKULA NA USHIRIKA WASIRA AAMUA KUSHONESHA SUTI KWA SHERIA NGOWI


BAADA ya kuandamwa sana katika mitandao ya kijamii kuhusu kutofunga vizuri vifungo vya suti yake,
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen Wasira ameamua kumuona mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ili aanze kumtengenezea suti zake.
Mhe. Wasira ameamua kukutana na mbunifu huyo aliyeanza mara moja kumchukua vipimo vyake ili amtengenezee mavazi yake ambayo atakuwa akiyatumia katika shughuli zake mbalimbali za kiserikali.
Kwa kuamua kumuona Sheria Ngowi, Mhe. Wasira atakuwa amepata mti shamba wa tatizo hilo lililotawala mitandao ya kijamii hivi karibuni. Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walirusha picha mbalimbali zikimuonesha Mhe. Wasira huku mmoja wa watangazaji akisema kuwa iwapo akikubaliwa, atajitolea kuwa Mbunifu wa suti zake za mitoko ili jambo hilo lisijitokeze tena.

 
Waziri Wasira akijaribu kurekebisha suti yake iliyokosewa kufungwa vifungo na kuzua mjadala mitandaoni.
Baadhi ya picha na katuni kutoka mitandaoni baada ya Mhe. Wasira kukosea kuvaa suti yake.

Mhe. Wasiara akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kanisa la Kisabato kwenye Uwanja wa Taifa, Dar huku koti la suti yake likiwa limekosewa kufungwa vifungo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...