Thursday, February 12, 2015

KITALE AAMUA KUUENZI UTEJA WAKE BONGO MOVIES




Moja ya kipeperushi kinachoonyesha namna ya kava ya movie hiyo itakavyo kuwa.
MCHEKESHAJI maarufu Bongo, Mussa Yusuph 'Kitale', hatimaye ameamua kuhamishia uteja wake ndani ya Bongo Movies kwa kuachia kideo kipya kitakacho kwenda kwa jina la Harusi ya Teja.
Akizungumza na mtandao huu hivi karibuni alisema kwamba ameamua kufanya filamu hiyo, ili Watanzania waweze kuona maovu yanayotokana na utumiaji wa Unga, kwani kufanya hivyo itakua ni njia moja wapo ya kuielimisha jamii kwa ujumla."Nawaomba wapenzi wangu wote wakae mkao wa kuipokea filamu yangu hii, kwani naamini kupitia hii wataweza kuelimika, hasa kwa wale ambao wanaona kutumia Unga ni ishu au ujanja basi kuanzia hapo wataacha kabisa kwani hakuna aliye mjanja kwa kujiingiza kwenye matumizi haya ya madawa ya kulevya", alisema Kitale.

Kitale akiwa katika moja ya mishemishe zake.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...