Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm amesema kuwa tayari amejua
janja ya wapinzani wao, BDF XI ya Botswana, kuelekea mchezo wa kesho wa
shirikisho Afrika ambapo amefunguka kuwa wanacheza soka la nguvu na la kukamia,
huku akiongeza kuwa tayari anajua ni ‘mwarobaini’ gani utawafaa hapo kesho.
Akizungumza na blogu hii, jana kwenye mazoezi ya kikosi chake
kwenye Uwanja a Taifa, Pluijm alisema amepata kila data na aina ya soka
wanalocheza ambapo alisema anaamini katika mchezo wa kesho watakuwa ni watu wa
kupaki basi ili wasubiri matokeo mazuri watakaporudiana wiki mbili baadaye.
“Nina habari zao nyingi sana, wanacheza soka la minguvu
‘physical’ wanakamia sana na ni wagumu ‘strong’ zaidi, lakini najua pia
wamekuja kwa lengo la kucheza soka la kujilinda zaidi ili iwe rahisi katika
mchezo wa marudiano.
“Hilo nimelitambua mapema na wiki nzima nimekuwa nikiwapa
mbinu nyingi washambualiaji kuhakikisha wanafunga mabao mengi ili kujiweka
katika mazingira mazuri katika mchezo wa marudiano,” alisema Pluijm.
No comments:
Post a Comment