Nani, aliyeinamia chini, akificha uso wenye machozi baada ya kufunga bao kali |
Winga wa zamani wa Manchester United, Luis Nani amemwaga machozi uwanjani kwa kuzidiwa na furaha baada ya kufunga bonge la bao, mita 30, wakati timu yake ya Sporting Lisbon ikiichakaza Gil Vicente mabao 2-0 juzi usiku.
Nyota huyo ambaye yupo Lisbon kwa mkopo akitoka Man United, ali-control mpira karibu na eneo la kona kabla ya kuachia fataki kali lililotinga wavuni moja kwa moja.
Nyota huyo ambaye yupo Lisbon kwa mkopo akitoka Man United, ali-control mpira karibu na eneo la kona kabla ya kuachia fataki kali lililotinga wavuni moja kwa moja.
Lakini hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyu, na
inaonekana ni tabia yake kumwaga chozi, ikikumbukwa aliwahi kumwaga chozi
uwanjani kwenye mchezo baina ya Man
United na Livewrpool baada ya Jamie Carragher kumchezea rafu, ilikuwa 2011 na
United kulala mabao 3-1 pale Anfield.
Carragher kwa ungwana alimfuata kwenye vyumba vya
kubadilishia nguo na kuomba radhi punde
baada ya mchezo kumalizika kabla ya Nani kufunguka kisa cha kulia siku hiyo kwa
kusema:
“Nilivyouona mguu wangu kwa mara ya kwanza, nilikuwa msimu
wangu ndo basi tena, ndiyo maana nililia sana, siku hiyo.”
Nani kushoto, enzi akiwa Man United akionesha jeraha baada ya kupigwa daruga na Carrager wa Liverpool. http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2964603/Nani-breaks-tears-scoring-Sporting-Lisbon-30-yard-stunner.html#v-4074974010001
No comments:
Post a Comment