Manchester United ipo katika harakati kambambe za kuhakikisha leo inanasa
saini ya nyota wawili kwa vyovyote kabla ya kufungwa kwa dirisha la
usajili mdogo leo usiku majira ya saa sita usiku.
Man U inataka kufanya kila linalowezekana kuhakikisha inamnasa
kiungo wa zamani wa Chelsea, Kelvin De Bruyne ambaye anakipiga Wolfsburg ya
Ujerumani, huku pia ikimuwinda kwa udi na uvumba, beki mahiri wa Borussia
Dortmund, Mats Hummels.
Licha ya Bruyne kushindwa kung’ara Stamford Bridge msimu uliopita na
kupelekwa Ujerumani, kiwango chake kimekuwa juu ambapo amekuwa nguzo wa
Wajerumani hao huku juzi akiiongoza timu yake kuichapa Bayern Munich mabao 4-1,
ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa Munich msimu huu kati ya mechi 18 ilizoshuka
dimbani mpaka sasa.
Van Gaal anaamini kumpata kiungo huyo raia wa Ubelgiji, kutasaidia kwa kiasi
kikubwa kuimarisha safu ya kiungo hususan katika mfumo wa 4-4-2 diamond (kupanua
uwanja).
Katika kukamilisha hilo, Van Gaal ametenga kiasi cha pauni milioni 30.
Katika kukamilisha hilo, Van Gaal ametenga kiasi cha pauni milioni 30.
Wakati huohuo, kocha huyo ametamka kuwa anahitaji huduma ya beki wa Dortmund, Hummels
licha ya kukiri itakuwa ngumu kumpata kutokana na klabu yake kutokuwa tayari
kumuachia katika kipindi hiki ambacho inapigana kujiokoa isishuke daraja katika
ligi kuu nchini Ujerumani.
Dortmund ambao ni mabingwa wa msimu 2012/13 wapo mkiani mwa ligi na
kocha Jurgen Klopp anapigana kuhakikisha timu hiyo haishuki daraja.
Katika kukamilisha dili hilo, Man U imemtengea kitita cha pauni milioni
37.
Duru za habari nyingine zinasema kuwa Man U wamemfungia kazi beki
tegemeo wa Paris Saint Germain (PSG) Marcos Correa ‘Marquinhos’ kwa kutenga
kitita cha milioni 35 kama watamkosa Hummels.
No comments:
Post a Comment