Bondia Francis Cheka (aliyenyanyua mkono), akiwa kwenye gari dogo la Magereza na baadhi ya wafungwa wengine muda mfupi baada ya kusomewa hukumu yake mapema leo katika  Mahakama ya 
Mkoa wa Morogoro,chini ya Hakimu wa Mahakama hiyo Said Musuya.
HATIMAYE Bondia maarufu wa 
ngumi za kulipwa Bongo, Francis Cheka amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela na 
kutakiwa kulipa fidia ya Sh. millioni 1 kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi
 meneja wa baa yake (Cheka) iitwayo Vijana Social iliyopo Morogoro 
Mjini.
Akimsomea mashitaka, Hakimu wa Mahakama ya 
Mkoa wa Morogoro, Said Msuya alisema Cheka alikutwa na hatia ya kumpiga 
aliyekuwa meneja wa baa yake aitwaye Bahati Kabanda 'Masika'.
Alisema kuwa Cheka alitenda kosa hilo Julai
 2, mwaka jana ambapo meneja huyo alikwenda kwenye baa hiyo kudai fedha 
zake alizokuwa hajalipwa na bondia huyo wakati akifanya kazi ya umeneja 
katika baa yake hiyo.
Hakimu Msuya alisema kuwa Cheka alikataa kumlipa na kumshushia kipigo kilichosababisha kulazwa hospitalini.
Baada ya hukumu hiyo huku Cheka 
akipandishwa kwenye difenda tayari kupelekwa gerezani akionekana 
kutokuwa na wasiwasi wowote, mashabiki wake walimvaa meneja huyo 
wakitaka kumshushia kipigo hivyo kuibua taharuki mahakamani hapo.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki hao 
walikuwa wakisema wapo tayari kujichanga ili kukata rufaa wakiamini kuwa
 bondia huyo ameonewa.
Mbali na hukumu hiyo mahakamani hapo, 
kulikuwa na kesi nyingine mbili zilizokusanya umati, moja ikiwa ni ya 
Sheikh Ponda juu ya uchochezi na ile ya mtoto wa boksi inayowakabili 
baba na mama Nasra
 Cheka akipanda kwenye gari la Magereza tayari kwa kwenda kutumikia kifungu hicho.
Mmoja wa Askari waliokuwa wamemuweka chini ya ulinzi Bondia huyo akimpokonya simu yake tayari kwa kwenda Gerezani.
 Cheka akijiandaa kudandia gari la Magereza.
...akimchimbia mkwara mmoja wa mapaparazi waliokuwa wakipiga picha za tukio hilo.
Askari akichukua baadhi ya vitu alivyokuwa navyo Bondia huyo.
No comments:
Post a Comment