Monday, June 2, 2014

TUKIO LA AJABU LINALOHUSISHWA NA USHIRIKINA KAZINI!



Gari la polisi likiwa eneo la tukio ambapo jamaa (aliyekaa chini kulia) aliyekumbwa na tatizo hilo akiwa chini akihangaika.


Ndani ya geti hili eneo la Legho, Sinza ndimo mwathirika wa chakula anamofanya kazi.

Mwathirika akisugua miguu chini kama vile anawashwa na vitu mwilini.

MTU mmoja ambaye anasadikiwa kula chakula na baadaye kuanza kuchanganyikiwa alinaswa na kamera yetu leo akisugua miguu ardhini na kujikuna mwili mzima, jambo ambalo lilidaiwa na wapita njia kuwa alikuwa amekula chakula kilichokuwa maalumu kwa ajili ya kafara.

Haikujulikana chakula hicho amekila wapi na ni chakula gani. Jina lake pia halikuweza kupatikana mpaka kamera yetu inaondoka sehemu hiyo.

Tukio zima limetokea eneo la Sinza-Legho Mtaa wa Shekilango, jijini Dar es Salaam, kwenye kampuni ya magari makubwa ya usafirishaji.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...