Askari wa usalama barabarani, Kinondoni, wakitoa maelezo kwa madereva wanaofanya safari za Makumbusho-Bagamoyo.
Mwonekano wa kituo kipya cha Makumbusho.
Stendi ya Makumbusho kabla haijaanza kutumika.
Mwenyekiti wa soko la Makumbusho, Bi Mary John (kulia), akiongea na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, SP Awadhi Haji (kati), na Mkuu wa Usalama Barabarani, Kituo cha Kinondoni, Solomon Mwangamilo (kushoto).
Huduma ya usafiri ikiendelea kama kawaida eneo la Makumbusho.
Mmoja wa madereva wa daladala akiuliza swali kwa viongozi wa usalama barabarani (hawako pichani).
Muonekano mpya wa kituo cha Mwenge baada ya kuhamishwa.
Barabara ya kuingilia Makumbusho kwa magari yanayotokea Kawe, Kunduchi, Bunju na maeneo hayo.
Shimo lililojaa maji katika njia ya kutokea daladala ziendazo Kunduchi, Kawe na Bunju.
Askari wa usalama barabarani wakiwa katika kituo kipya cha Makumbusho ili kutoa ushauri na miongozo.
Afisa Mfawidhi wa Sumatra Kanda ya Mashariki, Conrad Shio (kulia) akizungumzia kuhamishwa kwa kituo cha Mwenge kwenda Makumbusho.
Tangazo la kuhamishwa kituo cha Mwenge.
KAMERA yetu leo imeongea na wadau kuhusu kuhamishwa kwa kituo cha mabasi ya daladala kutoka Mwenge kwenda Makumbusho ambapo malalamiko yanahusu umbali wa kituo hicho kutoka maeneo ya abiria wengi na ubovu wa miundo mbinu sehemu hiyo kama ukosefu wa vyoo, vifaa vya kutupia uchafu na mashimo kwenye barabara kituoni na zile zinazoingia hapo.
Malalamiko mengine ni kwamba kituo ni kidogo mno, hakina alama muhimu za kuonyesha mabasi yanakokwenda.
Wengi walitaka barabara za hapo ziwekwe lami, na wengine wakataka nauli ya kutoka Bagamoyo iongezwe kwani mabasi sasa hayaishii Mwenge bali Makumbusho.
No comments:
Post a Comment