Friday, May 9, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA SIKU MBILI LA KUDHIBITI UJANGILI NA KUTOKOMEZA MAUAJI DHIDI YA TEMBO





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, asalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Hoteli ya Hyat Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam leo Mei 9, 2014 kwa ajili ya kufungua Kongamano la siku mbili la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo. Kongamano hilo linatarajia kumalizika kesho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, asalimiana na baadhi ya washiriki wa Kongamano la siku mbili la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Hoteli ya Hyat Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam leo Mei 9, 2014 kwa ajili ya kufungua Kongamano hilo linatarajia kumalizika kesho.





Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la siku mbili la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo. Kongamano hilo lililofunguliwa leo Mei 9, 2014, linatarajia kumalizika kesho kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Hyat Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.



Washiriki wa Kongamano hilo, wakisimama kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati alipowasili kufungua Kongamano hilo.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nakaaya Sumari, akiimba wimbo maalum wa kampeni ya kutomokeza mauaji ya Tembo, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la siku mbili la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo. Kongamano hilo lililofunguliwa leo Mei 9, 2014, linatarajia kumalizika kesho kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Hyat Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akizungumza wakati wa Kongamano hilo.




Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia kufungua rasmi Kongamano hilo, leo kwenye Hoteli ya Hyat Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo, baada ya kufungua rasmi leo kwenye Hoteli ya Hyat Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi kongamano hilo linalomalizika kesho kwenye Hoteli ya Hyat Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...