Saturday, May 10, 2014

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS JOSEPH KABILA LEO IKULU YA KINSHASA, AELEKEA ANGOLA



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ikulu ya Kinshasa leo.Rais Kikiwete alikuwa nchini DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili(picha na Freddy Maro)

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ikulu ya Kinshasa leo.Rais Kikiwete alikuwa nchini DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ikulu ya Kinshasa walipokutana kwa mazungumzo

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ikulu ya Kinshasa leo.Rais Kikiwete alikuwa nchini DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na Freddy Maro.

Rais Jakaya Kikwete amewasili mjini Kinshasa Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) usiku wa kuamkia leo kwa ziara ya kikazi akitokea nchini Nigeria ambapo amehudhuria Mkutano wa Viongozi kuhusu Uchumi barani Afrika.
Akiwa Kinshasa, leo tarehe 10 Mei, Rais Kikwete amefanya mazungumzo na Rais Joseph Kabila ambapo wanatarajia kuzungumzia uhusiano baina ya nchi mbili hizi na hali ya kisiasa kwa ujumla katika ukanda wa Jumuiya ya ushirikiano wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Mara baada ya Mazungumzo haya Rais Kikwete ameondoka kuelekea Luanda , Angola kwa ajili ya mazungumzo na Rais Jose Dos -Santos.

Wakati huo huo, Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Joyce Banda wa Malawi kufuatia kifo cha ghafla cha Balozi wa Malawi nchini Tanzania Flossy Gomile-Chidyaonga kilichotokea tarehe 9 Mei jijini Dar-Es-Salaam.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa Balozi Chidyaonga, ni huzuni kwetu sote" Rais amesema na kumuelezea Balozi Chidyaonga kuwa alikuwa mcheshi na aliyependa kushirikiana na wenzake kwa moyo mkunjufu.

" Ni huzuni zaidi kwetu sote kwakuwa kifo chake kimetokea ghafla mno kwa mtu tuliekua tunashirikiana naye kwa karibu katika juhudi za kukuza na kuimarisha mahusiano baina yetu" Rais amesema na kuongeza kuwa, kifo chake kimetokea wakati tunamhitaji zaidi na hivyo kusababisha pengo kubwa"

Rais amemuomba Rais Banda kufikisha salamu zake binafsi na za Watanzania kwa ujumla kwa familia ya marehemu, ndugu, Jamaa na Wamalawi wote kwa ujumla na kumuombea marehemu kwa mwenyezi Mungu, ampe mapumziko mema milele.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Kinshasa-DRC 10 Mei 14

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...