Monday, January 20, 2014

B12,ADAM MCHOMVU, DIVA WAREJESHWA CLOUDS FM



Mtangazaji wa Kipindi cha XXL Hamisi Mandi 'B12', akiwa katika pozi

WATANGAZAJI  Redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Hamis Mandi ‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’, hatimaye leo wameanza rasmi kuchapa kazi yao ya utangazaji baada ya kurejeshwa kwa mara nyingine kazini hapo kufuatia kusimamishwa na uongozi wa Clouds Media Group kwa takribani wiki tatu zilizopita,Watangazaji hao waliingia kwenye mgogoro na uongozi huo baada ya  kukiuka baadhi ya makubaliano na waajiri wao na kupelekea kuwapa adhabu hiyo, nakuwafanya wawe nje ya chumba cha kurushia matangazo ya redio hiyo, pamoja na kusimamishwa pia walitakiwa kuripoti kazini kila siku hadi leo ambapo wamesamehewa na kuanza kusababisha burudani kama ilivyokuwa mwanzo
Loveness Malinzi ‘Diva’. akiwa mzigoni tayari kwa kusababisha burudani zinazopatikana kupitia kipindi chake cha Ala za Roho ambapo hurusha matangazo yake kuanzia saa 4 usiku hadi saa 6 kamili.
 
Adam Mchomvu akitabasamu kwa pozi

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...